• info@demoinnovators.co.tz
 • +255 767 794 848, +255 766 193 544

Project Overview

Malengo makuu

Ni kuzalisha na kuuza mayai na kuku wa asili walio bora na wenye afya nzuri msimu mzima wa mwaka. Kuku hao watauzwa wakiwa na umri wa wiki 24 mpaka 28. Bei ya kuku mmoja ni shilingi elfu kumi (12,000 – 15,000) na mayai tireyi moja ni sawa yanauzwa shilingi elfu 12,000/

Malengo madogo

 1. Kuuza mayai na kuku wa asili.
 2. Pia kuuza mbolea ya kuku kwa wakulima.
 3. Kuuza vifaranga kwa wafugaji wadogo wadogo

Kutokana na ukweli kwamba uhitaji wa kuku wa asili ni mkubwa sana kulinganisha na uzalishaji wake, tunatarajia kuwa wazalishaji na wauzaji namba moja wa kuku wa asili katika eneo lote la jiji la arusha hivyo basi tutatoa huduma bora kwa wateja wetu wote na kwa bei rahisi kabisa

Sababu za msingi kabisa za kufanikiwa ni hizi:

 1. Kutengeneza mazingira yatakayokuwa tofauti na wazalishaji wengine ili kuwavutia wateja
 2. Kuwa na bei nafuu na za kawaida kwa huduma zetu zote

Jinsi tutakavyozalisha kuku wa asili

Utafiti na uzoefu unaonyesha kuwa kuku mmoja wa asili ana uwezo wa kutaga mayai kati ya 18-20 kwa msimu mmoja. Mradi unahitaji kuanza na kuku wazazi 222 yaani tetea 200 na jogoo 22 ili  kufikia lengo la kuzalisha kuku zaidi ya 7,000 na mayai 11,000 kwa kipindi cha miezi 11 ya uzalishaji.

Project Detail

 • Client Name:
  Bi. Christina
 • Client Company Name:
  Baraka Tele Group
 • Project Start Date:
  2021-06-01
 • Project End Date:
  2022-05-31
 • Client Comment:
  DEMO Innovators wametusaidia kuandika mpango wa mradi wenye kuleta tija na mafanikio kwa kikundi chetu cha akina mama.

Quick Contact

Recent Portfolio

See all our works that we do for our clients

Do you want to get our quality service for your business?