• info@demoinnovators.co.tz
  • +255 767 794 848, +255 766 193 544
News Photo

A newly book: Guide to Entrepreneur

Napenda kuchukua nafasi hii kuwasilisha wazo la kuandika mwongozo huu ambao utawaongezea wajasiriamali wetu waliorasimishwa na Mh. Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli baada ya kuwapa vitambulisho na kuwaruhusu kufanya biashara kwa uhuru bila bugudha yoyote. DEMO Innovators imekuja na wazo la kuandaa kitabu kidogo ambacho kitaitwa Mwongozo wa Ujasiriamali (JPM Maarifa) ambacho kitawaongezea wajasiriamali elimu na maarifa ya kufanya biashara.

Lengo kubwa ni kumuunga mkono na kumsaidia Mh. Rais kuwaongezea wajasiriamali ujuzi na maarifa yatakayo wawezesha kutatua changamoto wanazo kumbana nazo na pia kuwasaidia kuanzisha biashara, kufanya biashara au kuendeleza biashara zao kiubunifu, kiushindani na kujiajiri ili kupata mafanikio ya kuelekea uchumi wa kati wa nchi ya viwanda na hatimaye kutoka kwenye umachinga au hatua waliopo na kuwa wafanyabiashara wakubwa kwa badaye ambao wataleta “impact” (tija) katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kupambana na umaskini. 

Elimu hii itawajenga kuwa wajasiriamali wa kusimamia fedha zao, kuweka malengo na jinsi ya kutumia simu na mtandao kwa matumizi ya ujasiriamali.

Share This News

Comment

Do you want to get our quality service for your business?